• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatangaza kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia na Russia, na kusababisha wasiwasi na ukosoaji

    (GMT+08:00) 2019-02-02 17:25:21

    Serikali ya Marekani jana ilitangaza kuwa Marekani inajitoa kwenye makubaliano muhimu ya kudhibiti silaha na Russia, hatua ambayo inaonekana kuleta hatari ya kuwepo kwa ushindani wa silaha.

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo ametangaza hilo kwenye wizara ya mambo ya nje ya Marekani, akitolea mfano ukiukaji wa Russia wa makubaliano hayo, ambao unaifanya Russia iwe kwenye nafasi nzuri ya kijeshi na kuiweka Marekani pabaya.

    Baadaye jana Rais Donald Trump alisema Marekani itasonga mbele kuandaa machaguo yake ya kujibu kijeshi.

    Russia imeoneshwa kusikitishwa na uamuzi wa Marekani, na kusema hatua hiyo ilikuwa imeamuliwa zamani.

    Hata hivyo Bw. Pompeo amesema Marekani inaweza kubadilisha uamuzi wake baadaye, kama Russia itachukua hatua kufuata makubaliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako