• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujerumani na Ufaransa zatoa wito wa kudumisha mazungumzo ya kulinda "makubaliano ya kudhibiti silaha na Russia"

    (GMT+08:00) 2019-02-03 10:26:54

    Baada ya serikali ya Marekani kutangaza tarehe mosi Feburuari kwamba inajitoa kwenye "makubaliano ya kudhibiti silaha na Russia", kwa nyakati tofauti serikali za Ufaransa na Ujerumani zimetoa wito wa kulinda makubaliano hayo, na kudumisha mazungumzo. Hata hivyo NATO inasema inaunga mkono uamuzi huu wa Marekani.

    Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilitoa taarifa tarehe mosi usiku ikieleza kusikitishwa na Marekani kwa kujitoa kwenye makubaliano , na kuzitaka Ulaya na pande husika zilinde makubaliano ya sasa ya kudhibiti silaha. Taarifa hiyo inasema, katika kipindi cha miezi sita cha Marekani kujitoa kwenye makubaliano hayo, Ufaransa itazungumza kwa kina na nchi wanachama wa NATO, na kuhimiza kuendelea kufanya mazungumzo na Russia.

    Chansela wa Ujerumani Bibi Anjela Merkel alisema, Ujerumani itaendelea kuzungumza na Russia kuhusu makubaliano hayo katika kipindi hiki cha miezi sita. Na kwamba, bila kujali mazingira yoyote, atafanya kila awezavyo kuyafanya mazungumzo yafanyike tena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako