• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Muungano unaongoozwa na Marekani washambulia kituo cha kijeshi mashariki mwa Syria

  (GMT+08:00) 2019-02-03 16:01:08

  Televisheni ya taifa ya Syria imetangaza kuwa Muungano unaoongozwa na Marekani jana usiku ulilenga na kushambulia kituo cha kijeshi cha Syria kilichopo mashariki mwa Syria na kujeruhi askari wawili.

  Kulingana na ripoti, ndege za kivita za muungano huo zilishambulia kituo cha kijeshi cha Syria magharibi mwa mji wa al-Bukamal jimbo la Deir al-Zour la mashariki, na kufanya uharibifu. Hii si mara ya kwanza kwa Marekani kulenga vituo vya kijeshi vya Syria. Mwezi Mei, Juni na Disemba mwaka jana, muungano huo ulishambulia kwa mizinga maeneo ya kijeshi nchini Syria, na kusababisha uharibifu na majeruhi.

  Serikali ya Syria imeripotiwa kulaani mashambulizi hayo na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kumaliza vurugu zinazofanywa na Muungano huo nchini Syria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako