• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Misri lajadili kuongeza kipindi cha urais, na kuanzisha nafasi ya makamu wa rais

    (GMT+08:00) 2019-02-04 09:11:01

    Bunge la Misri limejadili kuongeza muda wa kipindi cha urais kutoka miaka minne hadi sita na kuanzisha nafasi ya makamu wa rais, kulingana na ombi rasmi lililosainiwa na kuwasilishwa na moja ya tano ya wabunge wote 596.

    Kamati kuu ya baraza la chini la bunge, ikiongozwa na spika Ali Abdel-Aal, imeeleza kanuni zitakazoongoza marekebisho ya katiba zikiwemo kurekebisha kasoro kubwa za kuwa na kipindi kifupi cha urais ambacho ni miaka minne na badala yake kukifanya kiwe miaka sita, pamoja na kuanzisha nafasi ya makamu wa rais ili kumsaidia rais katika majukumu yake. Kanuni hizo zitakazoongoza marekebisho yajayo ya katiba zimeliweka jeshi la Misri kuwa "mlinzi na mdhamini" wa demokrasia na hali ya kiraia nchini humo.

    Kamati pia imejadili kuanzishwa kwa seneti kama baraza la pili la bunge litakalofanya kazi sambamba na baraza la chini la bunge.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako