• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gor Mahia ya Kenya yaigaragaza Zamalek ya Misri kwa mabao 4-2 kwenye kombe la Shirikisho CAF

    (GMT+08:00) 2019-02-04 09:11:41

    Timu ya Gor Mahia ya Kenya jana iliwarambisha mchanga wageni wao ambao ni mabingwa mara tano wa kombe la Mabingwa wa Afrika Zamalek FC ya Misri kwa mabao 4-2 kwenye michuano ya kombe la Shirikisho CAF na kuendeleza ndoto zao za kuwa vinara wa hatua ya makundi.

    Mshambuliaji wa mbele wa Gor Mahia Jacques Tuyisenge alisaidia kuingiza magoli mawili katika kipindi cha kwanza na kumsaidia mshambuliaji Nicholas Kipkurui kufunga la tatu kabla ya Dennis Oliech akitokea benchi kuja kuiweka kifua mbele Gor Mahia kwa goli la nne dhidi ya waarabu wa Misri.

    Zamalek ilijibu kupitia Ibrahim Hassan ambaye naye pia alifunga mawili katika kipindi cha kwanza baada ya makosa yaliyofanywa na mlinda mlango wa Gor Mahia Bonifance Oluoch. Kwa ushindi huo sasa Gor Mahia wamekuwa vinara wa kundi D.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako