• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Afghanistan alishutumu wazo la Taliban la kuvunja jeshi

  (GMT+08:00) 2019-02-04 09:16:41

  Rais Mohammad Ashraf Ghani wa Aghanistan amelitaja wazo lililoripotiwa la kundi la Taliban la kulivunja jeshi la taifa baada ya makubaliano ya amani, kuwa ni njama dhidi ya vyombo vya usalama vya serikali yake.

  Sher Mohammad Abbas Stanikzai, mkuu wa zamani wa ofisi ya mawasiliano ya Taliban nchini Qatar aliyeongoza ujumbe wa mazungumzo wa Taliban katika mazungumzo na ujumbe wa Marekani yaliyofanyika hivi karibuni ameripotiwa kusema kuwa hakuna haja ya kuendelea kuwepo kwa jeshi nchini Afghanistan kama vikosi vya Marekani vitaondoka nchini humo.

  Rais Ghani amesema kwenye taarifa yake kuwa wazo hilo linalenga kuvunja vikosi vya usalama na ulinzi vya Afghanistan ili kudumisha hali ya kukosekana kwa utulivu na machafuko nchini Afghanistan, na kwamba amani isiyolindwa na vikosi vya usalama na ulinzi haikubaliwi na serikali.

  Kwa mujibu wa vyombo vya habari, mwakilishi maalumu wa Marekani anayeshughulikia upatanishi nchini Afghanistan Zalmay Khalizad aliyekutana na wajumbe wa Taliban mara nne tangu mwezi Novemba mwaka jana, amefikia makubaliano na kundi la Taliban, ambalo limeahidi kuwa litasimamisha vita kama serikali ya Marekani ikitangaza ratiba ya kuondoa vikosi vyake nchini Afghanistan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako