• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yazishutumu baadhi ya balozi kutokana na mawasiliano yao yasiyo ya kidiplomasia

    (GMT+08:00) 2019-02-04 09:17:06
    Serikali ya Afrika Kusini imekosoa kumbukumbu iliyotolewa na balozi za Marekani, Uingereza, Uholanzi, Ujerumani, na Uswisi inayoeleza ufuatiliaji wao kuhusu baadhi ya masuala nchini Afrika Kusini.

    Balozi hizo kwa pamoja zimemwandikia kumbukumbu rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini zikisema mpango wake wa kuhamasisha uwekezaji unaweza kushindwa kama asipochukua hatua dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka na vitendo vingine vya uhalifu. Pia zimeeleza wasiwasi wao kuhusu vizuizi dhidi ya uwekezaji wa kigeni kama vile mabadiliko katika kanuni za sekta ya madini.

    Msemaji wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano ya Afrika Kusini DIRCO Ndivhuwo Mabaya amesema balozi hizo hazifuati taratibu zinazotambuliwa kimataifa, na tume za kidiplomasia zinapaswa kuwasiliana na nchi zinakotumwa kwa njia ya barua ya kidiplomasia, na huko nchini Afrika Kusini ni kwa kupitia DIRCO. Amezitaka tume zote za kidiplomasia nchini Afrika Kusini kutoa barua rasmi kupitia njia mwafaka za kidiplomasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako