• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marais wa Russia, Uturuki na Iran kufanya mazungumzo huko Sochi

  (GMT+08:00) 2019-02-04 09:29:20

  Msemaji wa rais wa Russia Bw. Dmitri Peskov amesema, marais wa Russia, Uturuki na Iran watafanya mazungumzo tarehe 14 huko Sochi, mji uliopo kusini mwa Russia.

  Bw. Peskov amenukuliwa na gazeti la Izvestie la Russia akisema, marais wa nchi hizo tatu watajadili hali ya jimbo la Idlib nchini Syria, na swala la Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini Syria.

  Januari, 23 rais Vladimir Putin wa Russia na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan walifikiamakubuliano ya kuitisha mkutano mkuu wa nchi hizo tatu, ili kusukuma mbele mchakato wa ajenda ya Astana.

  Habari nyingine zinasema, rais Erdogan jana alisema, Uturuki inafanya mazungumzo ya ngazi ya chini na Syria, yanayohusu mambo ya sera ya diplomasia, ambapo idara ya ujasusi ya Uturuki imeshiriki kwenye mazungumzo hayo. Lakini rais Erdogan pia ameeleza, nchi yake haitafanya mazungumzo ya ngazi ya juu na Syria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako