• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Sudan wapongezana kuadhimisha miaka 60 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2019-02-04 18:24:34

    Rais Xi Jinping wa China na rais Omar Hassan Ahmed Al-Bashir wa Sudan leo wametumiana salamu za pongezi kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 60 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.

    Rais Xi Jinping amesema, katika miaka 60 iliyopita, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelezwa vizuri, ushirikiano katika pande mbalimbali umepata mafanikio makubwa. China inapenda kushirikiana na Sudan, kuzidisha ushirikiano wa sekta mbalimbali chini ya mfumo wa ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kutekeleza matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC, na kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Sudan kupata maendeleo makubwa zaidi.

    Rais Al-Bashir amesema, Sudan inapenda kuendelea kuimarisha urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, kuitikia wazo la kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya Sudan na China kuendelezwa kwenye kiwango cha juu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako