• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani kutuma askari zaidi ya 3,750 kwenye mpaka wa Mexico

  (GMT+08:00) 2019-02-04 18:27:37

  Wizara ya ulinzi ya Marekani (Pentagoni) imesema itatuma askari zaidi ya 3,750 katika mpaka wa Mexico kwa kipindi cha miezi mitatu ambao watajiunga na wengine na kufikia idadi ya askari 4,350 waliotumwa kusaidia kazi za mpakani humo.

  Hatua hiyo imekuja baada ya wabunge wanajaribu kujadili mkataba juu ya ufadhili wa usalama wa mpakani kwa lengo la kuzuia kufungwa kwa serikali kwa mara nyingine.

  Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akirudia mara kwa mara wazo lake la mwaka 2016 wakati wa kampeni za urais la kutangaza dharura ya kitaifa ikiwa mpango huo haujumuishi fedha kwa ajili ya kujenga ukuta wa mpaka na mexico.

  Mvutano kati ya Ikulu ya Marekani na wabunge wa Demokrati juu ya ufadhili wa ujenzi wa ukuta huo yalisababisha serikali kufungwa kwa siku 35 na kufika tamati Januari 25 mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako