• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatahadharisha mashambulizi kuwalenga wageni nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2019-02-04 18:56:18

    Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetoa tahadhari ya usalama kwa raia wa kigeni waishio nchini Kenya kutokana na hatari ya mashambulizi kwenye miji mitatu nchini humo.

    Katika taarifa yake, Ubalozi huo umetaka watu kuendelea kuwa waangalifu hasa katika maeneo ya mikusanyiko ikiwemo maeneo ya ibada, mahoteli na maduka makubwa na kueleza kuwa huenda magaidi wakapanga kushambulia wageni katika miji ya Nairobi, Naivasha na Nanyuki kaskazini mwa Kenya.

    Tahadhari hiyo inakuja muda mfupi baada ya kundi la Al-Shabab kushambulia hoteli na ofisi kadhaa mjini Nairobi Januari 15 na kuwaua watu 21 na wengine kujeruhiwa.

    Kundi la Al-Shabab limesema lilihusika na shambulizi lililotokea katika hoteli ya Dusit.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako