• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wa Tanzania waitaka serikali kuboresha bandari nchini

    (GMT+08:00) 2019-02-05 09:23:04

    Wabunge wa Tanzania wameitaka serikali kuiruhusu Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA kubakisha asilimia 40 ya makusanyo yake ya mwaka kwaajili ya kuboresha bandari nyingine za nchi hiyo.

    Wajumbe wa kamati ya bunge inayoshughulikia miundo mbinu wamesema serikali inapaswa kuiruhusu TPA kubakisha asilimia 40 ya dola zake milioni 117 zitokanazo na makusanyo ya mwaka kuboresha utendaji wa bandari za Dar es Salaam, Mtwara, Kigoma na Kalema. Akiwasilisha ripoti ya mwaka ya shughuli za kamati kuanzia mwezi Januari 2018 hadi Januari 2019, Mwenyekiti wa kamati, Moshi Kakoso amesema karibu mapato yote ya bandari yanakabidhiwa kwa serikali, na kuiacha mamlaka ya bandari ikose fedha katika utengenezaji mpya. Amesema bandari ya Dare es salaam ina changamoto nyingi zinazoathiri utendaji wake, zikiwemo kutokuwa na uwezo wa kushughulikia meli kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako