• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kufanya matangazo nchini China ili kuvutia zaidi uwekezaji

    (GMT+08:00) 2019-02-05 09:23:29

    Kenya inapanga kufanya matangazo nchini China ili kuvutia zaidi uwekezaji nchini.

    Akiongea na Shirika la habari la China Xinhua, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji ya Kenya (KenInvest) Moses Ikiara, amesema timu ya maofisa wa sekta za umma na binafsi watatembelea mikoa mitatu ya hapa China mwezi Machi, wakiwa na lengo la kuwavutia wawekezaji wa China kuwekeza kwenye sekta za utengenezaji, hasa viwanda vya nguo, ujenzi, biashara ya kilimo, na ngozi. Bw. Ikiara amesema China ni miongoni mwa vyanzo vikukuu 10 vya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje nchini Kenya.

    Wakati huohuo Kenya inataka kusaini makubaliano ya utengezaji wa filamu na China ili kupanua sekta ya filamu ya Kenya. Kwa mujibu wa waziri wa teknolojia ya habari na mawasiliano wa Kenya Joe Mucheru, Kenya imezindua mashindano ya filamu ambayo yataiwezesha nchi kutengeneza filamu zenye ubora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako