• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw. Lavrov asema kujitoa kwa Marekani kwenye Mkataba wa INF kutapunguza masharti ya matumizi ya silaha za nyuklia

  (GMT+08:00) 2019-02-05 09:45:22

  Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov amesema kujitoa kwa Marekani kwenye mkataba wa makombora ya nyuklia ya masafa ya kati INF kutapunguza masharti ya matumizi ya silaha za nyuklia na kuongeza hatari za kutokea kwa mgogoro wa nyuklia.

  Bw. Lavrov amesema hayo wakati akiwa kwenye ziara yake nchini Kyrgyzstan. Ameongeza kuwa lengo la Marekani kujitoa kwenye mkataba wa INF ni kuharibu mfumo wa kudhibiti vifaa vya silaha na kupunguza silaha za kimkakati, na Russia bado ina nia ya kufanya mazungumzo na Marekani kwa misingi ya usawa na manufaa ya pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako