• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Guterres asema Umoja wa Mataifa utaziunga mkono serikali za nchi husika katika kutatua shughuli za mamluki

  (GMT+08:00) 2019-02-05 09:50:46

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, Umoja huo uko tayari kuendelea kuziunga mkono serikali za nchi husika katika kutatua shughuli za mamluki.

  Akihutubia mazungumzo ya ngazi ya juu ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Bw. Guterres amesema kuwepo kwa askari mamluki na wapiganaji wa kigeni kunafanya mizozo kuzidi kuwa migumu kutatuliwa na kunatishia utulivu, mambo ambayo yanadhoofisha utawala wa sheria na kuendeleza uovu. Bw. Guterres ameongeza kuwa, shughuli za mamluki zinatia hofu kubwa zaidi, na kutaka kuongeza juhudi ili kukabiliana na matatizo yote yanayohusiana na shughuli za mamluki ikiwemo kuimarisha utawala wa kisheria. .

  Habari zaidi zinasema kuwa, mwakilishi maalum wa rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu ameeleza kwenye mazungumzo kuwa, China siku zote inaunga mkono juhudi za nchi za Afrika za kujipatia amani na utulivu, ustawi na maendeleo, na inaiunga mkono Afrika kutekeleza Ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika na Pendekezo la kutotumia silaha za bunduki ifikapo mwaka 2020. China imeamua kuanzisha mfuko wa ushirikiano wa amani na usalama kati ya China na Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako