• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda yaomba kurejelea uzaji wa kuku nje ya nchi

    (GMT+08:00) 2019-02-05 18:36:27
    Uganda imewasilisha ripoti kwenye shirika la afya ya mifugo duniani OIE kwamba imeangamiza kabisa homa ya ndege na hivyo inaweza kurejelea uuzaji wa kuku kwenye masoko ya kikanda.

    Awali mwaka 2017 uuzaji wa kuku wa Uganda ulikuwa umepigwa marufuku kwenye kanda ya Afrika mashariki baada ya kuzuka kwa homa hiyo.

    Katibu wa kudumu kwenye wizara ya mifugo nchini Kenya Harry Kimutai sasa wanasubiri ripoti ya OIE ili kuondoa marufuku ilioko.

    Mbali na Kenya, Uganda pia huuza bidhaa zake za kuku nchini Rwanda na Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako