• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Startimes yakamilisha mradi wa dijitali Uganda

    (GMT+08:00) 2019-02-05 18:36:58
    Serikali ya China imekamilisha mradi wa uhamiaji kutoka mfumo wa runinga wa analojia kwenda dijitali nchini Uganda.

    Mradi huo unatarajiwa kufaidi vijiji 500 nchini humo.

    Mradi huo kwa jina Access to Satellite TV ni sehemu ya mpango mpana wa kuleta huduma za runinga yenye mfumo wa dijitali kwa zaidi ya vijiji 10,000 bwarani Afrika.

    Umetekelezwa na kampuni ya Star Times chini ya usimamizi wa ubalozi wa China nchini Uganda na wizara ya mawasiliano nchini humo.

    Msahauri wa kiuchumi kwenye ubalozi wa China nchini Uganda bibi Zheng Xiu Fen, amesema mradi huo ni ishara kwamba ushrikiano wa zaidi ya miaka 56 ya kibishara unakua siku hadi siku kwenye miradi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako