• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Kigali kuwania tuzo la mji bora

  (GMT+08:00) 2019-02-05 18:39:22

  Mji mkuu wa Rwanda, Kigali umechaguliwa miongoni mwa miji 16 kwa toleo la kwanza la Tuzo za Wellbeing City, tuzo ambayo inatambua miji inayozingatia maisha bora ya wakaazi kwenye upangaji wake.

  Kigali iliyochaguliwa katika kitengo cha afya ya jamii ni mji pekee wa Afrika kwenye tuzo hizo.

  Uteuzi wa Kigali ulihusishwa na sera ya siku ya kutotumia gari mara mbili kwa mwezi ambayo ili kusaidia wakaazi kufanya mazoezi ya mwili.

  Zaidi ya miji 100 kutoka nchi 27 na mabara sita ilichaguliwa kwa ajili ya tuzo hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako