• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Bunge latoa mwongozi kuhusu uagizaji wa sukari Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-02-05 18:37:56
    Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira nchini Tanzania imekosoa utaratibu wa utoaji wa vibali vya kuingiza sukari ambapo imesema vimekuwa vikitolewa bila kuzingatia upungufu wa sukari iliyopo kwa wakati husika.

    Mwenyekiti wa kamati hiyo, Suleiman Saddiq amesema swala hilo linatoa mianya kwa wafanyabiashara wasio waaminifu kuamua kupunguza uzalishaji na kuingiza sukari zaidi ya kutoka nje ya nchi.

    Amesema kwa kuwa hatua ya kupunguza uzalishaji ina madhara katika ajira, Bunge linaishauri Serikali kabla ya kutoa vibali kwa mwaka 2019 ifanye tathimini upya kwa lengo la kubaini uwezo wa viwanda ndani na upungufu wa sukari.

    Amesema hatua hiyo itasaidia kubaini mahitaji halisi lakini pia kujua sifa za waombaji na kuondoa hali ya sintofahamu inayoendelea sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako