• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe wa Marekani kutembelea Korea Kaskazini kuandaa mkutano wa Trump na Kim

  (GMT+08:00) 2019-02-05 18:40:29

  Mjumbe maalumu wa serikali ya Marekani Bw. Stephen Biegun anatarajiwa kwenda Pyongyang Korea Kaskazini kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa pili kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Bw. Stephen atawasili Korea Kaskazini kesho na atakutana na mwenzake wa Korea Kaskazini Bw. Kim Hyok Chol kabla ya viongozi wa nchi hizo mbili hawajakutana.

  Mkutano wa viongozi hao ni maendeleo ya mazungumzo ya awali yaliyofanyika nchini Singapore ikiwa na lengo la kudumisha uhusiano wa nchi hizo mbili na kujenga amani ya kudumu ya Peninsula ya Korea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako