• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina walioko nje ya nchi wafurahia tamasha la mwaka mpya wa jadi wa kichina lililoandaliwa na CMG

    (GMT+08:00) 2019-02-05 18:41:19

    Kutazama tamasha lililoandaliwa na CMG ni shughuli isiyokosekana ya wachina wote duniani katika mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa kichina. Barani Afrika, wachina wakiwemo askari wa kulinda amani, madaktari wanaotoa msaada, wajenzi wa miundombinu wamefurahia tamasha hilo la mwaka huu.

    Bw. Li Haifeng wa Kampuni ya Ujenzi ya Anhui ya China anafanya kazi nchini Kenya. Amesema aliposikia wimbo wa tamasha hilo, aliona kama yupo nyumbani. Anasema,

    "Tamasha la mwaka huu ni zuri sana. Sisi watu walioko nje ya China tunapenda kutazama tamasha hilo, kwani familia yetu pia wanalitazama nchini China wakati huo huo."

    Huu ni mwaka wa tatu kwa Bi. Yang Yu kusheherekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina nchini Kenya. Anasema,

    "Katika tamasha la mwaka huu, tumewaona nyota wengi wa filamu na tamthilia. Tulipotazama tamasha hilo tuliona kama tuko nyumbani."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako