• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Spika wa bunge la Uganda azitaka shule kufundisha lugha ya kichina

    (GMT+08:00) 2019-02-06 09:40:43

    Spika wa bunge la Uganda Rececca Kadaga amezitaka shule za nchi hiyo kufundisha lugha na utamaduni wa kichina.

    Akitembelea shule ya kimataifa ya St. Michael, Kadaga amesema watu wa Uganda wanapaswa kujifunza lugha ya kigeni zaidi ya moja, na kujifunza lugha ya kichina kunaweza kuongeza fursa kwa wazawa kufanya kazi katika makampuni ya China na pia kufanya biashara nchini China. Ameeleza kuwa kitu kinachowazuia watu wa Uganda kupata nafasi za ajira kutoka nchi nyingine ni tatizo la lugha na kusema hii ndio sababu ya kuwahamasisha watu wa Uganda kujifunza lugha za kigeni, haswa kichina, kwani kuna wawekezaji wengi wa kichina nchini Uganda, ambao wanahitaji watafsiri ili waendeshe biashara zao nchini humo.

    Kwa mujibu wa mpango uliotolewa mwaka jana na Kituo cha Taifa cha Maendeleo ya Mtaala, kuanzia mwezi huu shule za sekondari zilizochaguliwa zinatarajiwa kuanza kufundisha lugha ya kichina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako