• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wa Tanzania watoa tahadhari juu ya uwezekano wa kurejea tena kwa ujangili

    (GMT+08:00) 2019-02-06 09:41:10

    Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wametoa tahadhari juu ya uwezekano wa kurejea tena kwa ujangili wa tembo kutokana na mabadiliko ya mfumo wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii.

    Mwaka 2017 serikali ya Tanzania ilifuta umiliki wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii na kutangaza maandalizi ya mfumo mpya wa kutoa vibali kupitia mnada wa ndani ya siku 60. Mjumbe wa kamati hiyo Stephen Kiruswa ameliambia bunge mjini Dodoma kuwa serikali imeshaanza kuona madhara ya uamuzi huo kwani idadi kubwa ya wawekezaji wamerejesha vitalu vingi vya uwindaji kwa serikali. Ameongeza kuwa mapato yanayotokana na vitalu vya uwindaji pia yamepungua kutoka dola milioni 27 za mwaka 2008 hadi milioni 8 za mwaka 2018.

    Ameishauri serikali kuchukua hatua za haraka ili kuokoa sekta ya utalii kwa kuwapa wawekezaji wanaostahili leseni ya miaka mitano kutoka mwaka 2018 hadi 2022 ili kurejesha hasara iliyotokea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako