• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaimarisha usalama mjini Naivasha kufuatia tahadhari ya ugaidi

    (GMT+08:00) 2019-02-06 09:41:35

    Maofisa wa usalama nchini Kenya wamesema wameimarisha doria kwenye mji wa Naivasha kutokana na tahadhari ya ugaidi iliyotolewa na ubalozi wa Marekani nchini Kenya.

    Akiongea na wanahabari mjini Naivasha, Kamishna wa kaunti ndogo ya Naivasha Jim Njoka, amewahakikishia watalii wa kigeni na wakazi wa huko kwamba wameweka usalama wa kutosha huko Naivasha na kuwataka wakazi kushirikiana na maofisa wa usalama kutoa taarifa endapo wataona tabia zozote zinazotia mashaka mjini. Amesema tangu Disemba mwaka jana maofisa wa usalama wamekuwa wakichukua tahadhari kubwa na wataendelea na utaratibu huo katika mji mzima na hata kwenye vituo vikubwa.

    Ubalozi wa Marekani nchini Kenya Jumatatu ulitaja miji ya Nairobi, Naivasha, Nanyuki na miji ya pwani kuwa ni miji inayolengwa na magaidi na kuwashauri wakazi kuwa na tahadhari kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako