• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Morocco:Wasio na ajira wapungua Morocco

    (GMT+08:00) 2019-02-06 15:18:07
    Idadi ya watu wasiokuwa na ajira nchini Morocco imeendelea kushuka na kufikia asilimia 9.8 mwaka 2018 ikilinganishwa na asilimia 10.2 ya mwaka 2017.

    Ripoti ya shirika la mipango zinaonyesha kuwa uchumi ulisaidia kuzalishwa kwa kazi mpya 112,000 mwaka 2018 ikiwemo kazi 21,000 kwenye maeneo ya mashambani.

    Sekta ya huduma ilizalisha ajira 65,000, ujenzi 15,000 na utengenezaji bidhaa ajira 13,000.

    Nayo sekta ya kilimo ilisaidia kupatikana kwa ajira 19,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako