• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Gasmeth kuwekeza dola milioni 400 kwenye mradi wa gesi ziwa Kivu

    (GMT+08:00) 2019-02-06 15:19:23
    Kampuni ya Gasmeth Energy Limited, imeahidi kuwekeza dola milioni 400 kwenye mradi wa gesi ya methane katika ziwa Kivu nchini Rwanda.

    Kampuni hiyo imesaini makubaliano na serikali kupitia kwa halmashauri ya madini, petroli na gesi na halmashauri ya maendeleo nchini humo.

    Mradi huo utahusisha uzalishaji wa kawi kwa kutumia gesi hiyo huku serikali ikilenga kutoa huduma za umeme kwa wote ifikapo mwaka 2020.

    Uwekezaji huo unatarajiwa kufungua nafasi za ajira kwa kati ya watu 600-800.

    Mkurungezi wa halmashauri ya maendeleo Clare Akamanzi amesema gesi asilia haina athari yoyote kwa mazingira na itasaidia kupunguza matuizi ya kuni na makaa kwa shughuli za upishi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako