• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar : Rais wa Zanzibar asifu ushirikiano na Misri kwenye kilimo

    (GMT+08:00) 2019-02-06 15:19:39
    Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesifu juhudi zinazochukuliwa na Misri ya kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya kilimo.

    Akizungumza na Waziri wa Kilimo na Masuala ya Ardhi wa Misri, alisema kuwa Misri imekuwa mshirika mkubwa wa Zanzibar katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuimarisha maendeleo.

    Dk. Shein alieleza kuwa azima ya serikali ya Misri ya kuendeleza ushirikiano katika uendelezaji wa mradi wa shamba la pamoja la Jeshi la Kujenga uchumi Zanzibar (JKU) huko Bambi umeleta tija na maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo.

    Alieleza miongoni mwa mafanikio yaliopatikana ni pamoja na kuwapo kwa wataalamu na utaalamu unaotokana na msaada wa Misri, ambapo juhudi hizo zimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza sekta ya

    kilimo hasa katika mradi huo.

    Naye Waziri wa Kilimo na masuala ya Ardhi wa Misri, Dk. Ezzaldin Abusteit, alimweleza Dk. Shein, azima ya serikali ya nchi hiyo ya kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako