• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kebs yasimamisha vibali vya kampuni za siagi

    (GMT+08:00) 2019-02-06 15:19:57
    Shirika la kukadiria ubora wa bidhaa nchini Kenya KEBS imesimamisha vibali vya kampuni za bidhaa za siagi za karanga baada ya kugundua kuwa zimezidisha kiwango cha sumu kwenye bidhaa zao.

    Kebs imesema kampuni hizo ni pamoja na Triclover na Mother's Nature ambazo tayari zimeagizwa kusimamisha uzalishaji wake wa siagi.

    Utafiti wa maabara wa Kebs umeonyesha kuwa bidhaa za kampuni hizo zimepitisha kiwango cha aflotoxin kinachotakiwa cha sehemu 15 kwa bilioni .

    Awali aina nyingine ya siagi ya Nuteez iliondolewa madukani kufuatia kugunduliwa kwa sumu inayoweza kusababisha saratani.

    Mkurugenzi wa Afya ya Umma Kepha Ombacho alisema kiwango cha aflotoxin kwenye siagi hiyo ya karanga ilikuwa zaidi ya mara mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako