• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani atetea udhibiti wa mipaka katika hotuba yake kuhusu mambo ya kitaifa

    (GMT+08:00) 2019-02-06 18:55:56

    Rais Donald Trump wa Marekani jana alipohutubia bunge kuhusu mambo ya kitaifa akitetea kuimarisha udhibiti wa mipaka, na kuwazuia wahamiaji haramu.

    Rais Trump amesema bunge hilo lina siku 10 tu katika kuidhinisha muswada wa kuimarisha udhibiti wa mipaka. Amesisitiza kuwa suala la wahamiaji haramu ni mgogoro mkubwa zaidi kati ya raia na wanasiasa nchini Marekani. Amesema wanasiasa tajiri wana ukuta na walinzi, hivyo wanataka kufungua mpaka, lakini raia wa kawaida wanakabiliwa na changamoto za ajira na kipato cha chini kutokana na suala la wahamiaji haramu.

    Kuhusu mambo ya kidiplomasia, rais huyu amesema Marekani inatekeleza sera yenye kanuni kuhusu suala la Mashariki ya Kati, na itapunguza wanajeshi wake nchini Syria na Afghanistan. Aidha, amesema Iran ni nchi inayotoa uungaji mkono zaidi kwa makundi ya kigaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako