• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi    Maongezi ya upendo kati ya Xi Jinping na wazee

  (GMT+08:00) 2019-02-07 08:12:26

  Kwenye vitabu vilivyochapishwa, tuliona picha mbili kati ya picha chache za familia ya Rais Xi Jinping zilizotolewa hadharani. Moja ni ya Xi Jinping na wanafamilia wake, ambapo Xi anasukuma kiti chenye magurudumu alichokaa baba yake mzazi, na picha nyingine ni Xi Jinping amemshika mkono wa mama yake mzazi wakiwa wanatembea kwa miguu. Kutokana na hali ya familia yake, Xi Jinping anafuatilia sana suala la kuongezeka kwa idadi ya wazee kwenye jamii ya China, na namna ya kumwezesha kila mzee aishi vizuri maisha ya uzeeni. Katika kipindi hiki cha Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi, leo tunawaletea makala ya tatu: Maongezi ya upendo kati ya Xi Jinping na wazee:

  Mzee: Sisi tumenufaika kutokana na msaada wa wewe rais wetu!"

  Xi Jinping: Sisi sote tunatarajia kupata afya nzuri na kuishi maisha marefu, ninawatakia muwe na furaha kila siku, na kufurahi daima!"

  Hayo ni maongezi kati ya mzee mmoja wa kawaida wa Shanghai na Rais Xi aliyemtembelea. Hivi sasa jamii ya China inakabiliwa na tatizo la kuongezeka kwa idadi ya wazee. Inakadiriwa kuwa, kabla na baada ya mwaka 2050, idadi ya wazee nchini China itafikia milioni 487 ambayo ni asilimia 34.9 ya idadi ya jumla ya watu. Tangu achaguliwe kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama mwaka 2012, Xi Jinping ametembelea mara kwa mara nyumba za matunzo ya wazee wa aina mbalimbali na kuwatembelea wazee, na kufanya utafiti kuhusu maendeleo ya mambo ya matunzo ya wazee nchini China.

  Mkesha wa Siku ya kwanza ya Mwaka mpya wa 2014, Xi Jinping alitembelea Nyumba ya matunzo ya wazee ya Sijiqing kwenye Eneo la Haidian mjini Beijing, ambapo aliongea na Bw. Liu Zhong'an na mke wake Zhang Junqiu wenye umri wa zaidi ya miaka 80:

  Xi Jinping: Kwanini mnapenda kuishi katika nyumba hii?

  Mzee: Hapa tunaweza kupata urahisi wa matibabu, hata kila kitu kinaweza kufanyika tukiwa vitandani. Hatuna taabu ya kupata chakula, na tunaweza kushiriki kwenye shughuli mbalimbali.

  Xi Jinping: Watoto wenu wanakuja kuwatembelea mara kwa mara?

  Mzee: Wanakuja kila wiki.

  Xi Jinping: Mnaweza kurudi nyumbani kwenu baadaye?

  Mzee: Sitaki kurudi nyumbani tena, kwani nimezoea maisha ya hapa.

  Xi Jinping: Ninawatakia maisha ya furaha !

  Shanghai ni mji mkubwa kupita kiasi ambao uliingia mapema kuliko miji mingine nchini kwenye jamii yenye idadi kubwa zaidi ya wazee, hata kwenye eneo lake la Hongkou, idadi ya wazee imechukua asilimia 40. Tarehe 6 Novemba,2018, Xi Jinping alitembelea kituo cha kuwatunza wazee wakati wa mchana kwenye eneo hilo, alipozungumza na wazee alieleza matarajio yake:

  "Suala la kuongezeka kwa idadi ya wazee linafuatiliwa zaidi na serikali kuu. Sasa tumeingia kwenye jamii yenye idadi kubwa ya wazee, maisha ya furaha ya wazee ni muhimu sana kwenye maisha ya furaha ya wananchi, sasa kazi ya matunzo ya wazee inaendeleaje? Afya ya wazee ni ya namna gani? Yote hayo tunayafuatilia sana. Nimeona wazee wa hapa wanafuraha sana, ninawatakia waishi kwa furaha kila siku na kufurahi daima!"

  Namna ya kutekeleza kihalisi sera kuhusu matunzo ya wazee na kuwanufaisha zaidi wazee, ni suala ambalo kiongozi huyu mkuu wa China alinafuatilia kila wakati. Mwaka 2013 alipotembelea nyumbani kwa bikizee kwenye Kijiji cha Shi Ba Dong kilichoko mbali sana mlimani katika Mkoa wa Hunan, Bi kizee Shi Pazhuan mwanzoni hakutambua kuwa ni rais alikuja kumtembelea, baadaye aliambiwa walipoongea:

  Xi: Wewe ni mkubwa kama dada yangu, mimi ningekutembelea zaidi.

  Mzee: Wewe ni kiongozi mkuu, ni ofisa mkuu unayetufuatilia sisi raia.

  Xi: Mimi ni mtumishi wa wananchi."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako