• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN yasema maelfu ya wakimbizi nchini Uganda wanakosa elimu

    (GMT+08:00) 2019-02-07 09:19:25

    Wakati muhula mpya wa masomo ukianza nchini Uganda, Shirika la Kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeonya kuwa maelfu ya wakimbizi wanakosa elimu kutokana na ukosefu wa fedha.

    Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Uganda Joel Boutroue, amesema asilimia 60 tu ya wakimbizi watoto ndio wanaweza kupata elimu ya msingi na madarasa yanajaa wanafunzi huku mwalimu mmoja akiwafundisha watoto zaidi ya 100. Boutroue amesema asilimia 12 tu ya watoto waliomaliza shule ya msingi ndio wanaweza kupata elimu ya sekondari kwasababu wengine hawana rasilimali muhimu. Amebainisha kuwa wale wanaokosa elimu ya sekondari wanasababisha matatizo makubwa, kwani wanaishia kutofanya chochote na kujiingiza kwenye tabia hatarishi.

    Hata hivyo amesema mpango wa wakimbizi mwaka huu unahitaji dola za kimarekani bilioni moja ili kuweza kuendelea kutoa usaidizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako