• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Palestina atumai kuwa uchaguzi wa Israel utaleta uongozi mpya unaoamini amani

  (GMT+08:00) 2019-02-07 09:29:41

  Rais Mahmoud Abbas wa Palestina ameeleza matumaini yake kuwa uchaguzi wa wabunge wa Israel utakaofanyika mwezi Aprili utaleta uongozi mpya unaoamini amani.

  Rais Abbas amesema hayo kwenye mkutano wa Baraza la Amani na Uhuru la Palestina uliofanyika jana mjini Ramallah, ambapo alisisitiza kuwa anaamini imani na hataki vita. Ameongeza kuwa bila ya ufumbuzi wa suala la Palestina, hakutakuwa na amani na usalama katika kanda hiyo na dunia nzima. Mkutano huo ulioanza mwezi Januari umewakutanisha wabunge, wasomi na watu wengine mashuhuri ili kuunga mkono suluhu ya mataifa mawili katika msingi wa mpaka ulioamuliwa mwaka 1967.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako