• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UN yatoa wito wa kutokomeza ukeketaji dhidi ya wanawake ifikapo 2030

  (GMT+08:00) 2019-02-07 09:59:14

  Wakuu wa mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kuchukua hatua za kutokomeza ukeketaji dhidi ya wanawake ifikapo 2030.

  Wito huo wameutoa kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji. Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Henrietta Fore, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa UNFPA Natalia Kenem, na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake UN Women Phumzile Mlambo-Ngcuka, imesema wasichana na wanawake wasiopungua milioni 200 walio hai wamekeketwa, wakiteswa na vitendo vya ukatili mkali zaidi dhidi ya jinsia duniani. Pia wamesema ukeketaji hautakuwa salama kamwe bila kujali unafanywa na nani na wapi..

  Mwaka 2015 viongozi wa nchi mbalimbali duniani waliunga mkono kutokomeza ukeketaji dhidi ya wanawake ifikapo mwaka 2030 kuwe moja kati ya malengo ya Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030. Taarifa hiyo imesema, ni lazima hatua ichukuliwe sasa, ili kugeuza dhamira hiyo ya kisiasa na kuwa vitendo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako