• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ubalozi wa China nchini Marekani waandaa tafrija ya kuadhimisha mwaka mpya wa jadi wa kichina

  (GMT+08:00) 2019-02-07 18:47:18

  Ubalozi wa China nchini Marekani umeandaa tafrija ya kuadhimisha mwaka mpya wa jadi wa kichina pamoja na miaka 40 tangu China na Marekani zianzishe uhusiano wa kibalozi.

  Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiakai amesema huu ni mwaka wa 40 tangu China na Marekani zianzishe uhusiano wa kibalozi. Katika miaka 40 iliyopita, uhusiano huo umehimiza maendeleo ya nchi hizo mbili, na kuwanufaisha wananchi wao. China na Marekani zimedumisha uratibu na ushirikiano katika mambo ya kimataifa, nakutoa mchango muhimu kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa dunia. Ameongezakuwa uzoefu wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika miaka 40 iliyopita umethibitisha kuwa ushirikiano unaleta manufaa, na upinzani unaleta hasara kwa pande hizo zote.

  Wajumbe karibu 750 wa hali mbalimbali wakiwemo waziri wa biashara wa Marekani, naibu waziri wa uchukuzi wa nchi hizo wamehudhuria tafrija hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako