• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yatakiwa kusimamia na kuhimiza upandaji miti

    (GMT+08:00) 2019-02-07 18:58:08

    Wafanyabiashara wa mkaa wilayani Handeni mkoani Tanga Tanzania wamesema serikali imechelewa kuhimiza wananchi katika suala la kupanda ili kulinda uoto wa asili kutokana na maeneo mengi kuathirika baada ya miti kukatwa kwa ajili ya kupata mkaa na mbao.

    Wafanya biashara hao wamesema kwa sasa Serikali inatakiwa kusimamia na kuhimiza upandaji miti kwa wingi kwa kuwa tayari kuna maeneo ambayo mazingira yake yameshaathirika kutokana na kukatwa miti.

    Mmoja wa wauza mkaa wa Mtaa wa Zizini, Suphian Rashid anasema maeneo kama Kijiji cha Kwankonje kilichoko Kata ya Kwamsisi mpaka Kwasunga, misitu yake imeharibiwa na wananchi ambao wanazalisha mbao na mkaa.

    Serikali imetakiwa kuweka mkakati ili gesi ipungue bei, wananchi waone kutumia mkaa ni gharama kuliko gesi ili misitu ilindwe.

    Anasema mkaa ni biashara endelevu kwao kwa kuwa una wateja wengi kutokana na ukweli kwamba mtu wa hali ya chini na mwenye uwezo, wote wanatumia mkaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako