• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utaratibu wa utoaji vibali vya kuingiza sukari Tanzania wakosolewa

    (GMT+08:00) 2019-02-07 18:58:25

    Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imekosoa utaratibu wa utoaji wa vibali vya kuingiza sukari ambapo imesema vimekuwa vikitolewa bila kuzingatia upungufu wa sukari iliyopo kwa wakati husika.

    Mwenyekiti wa kamati hiyo, Suleiman Saddiq ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya shughuli za kamati hiyo kwa kipindi cha kuanzia Machi, 2018 hadi Januari, 2019 kwa Bunge.

    Amesema jambo hilo linatoa mianya kwa wafanyabiashara wasio waaminifu kuamua kupunguza uzalishaji na kuingiza sukari zaidi ya kutoka nje ya nchi.

    Bunge la Tanzania limeishauri Serikali kabla ya kutoa vibali kwa mwaka 2019 ifanye tathimini upya kwa lengo la kubaini uwezo wa viwanda ndani na upungufu wa sukari.

    Amesema hatua hiyo itasaidia kubaini mahitaji halisi lakini pia kujua sifa za waombaji na kuondoa hali ya sintofahamu inayoendelea sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako