• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa KRA wafanya msako wa kuwakamata wakwepaji ushuru

    (GMT+08:00) 2019-02-07 18:59:01

    Idara ya polisi kwa ushirikiano na maofisa wa mamlaka ya Kodi Kenya KRA wamefanya msako katika kampuni ya Mvinyo ya African Spirit Distillers, Thika na kuwatia nguvuni mameneja watatu kwa kukwepa ulipaji wa Kodi. Kikundi hicho kilichoongozwa na afisa mkuu wa kitengo cha Flying Squad Bw Musa Yego, na naibu kamishna wa KRA Bi Anne Nyaguthie Irungu, kilipata fununu kutoka kwa wananchi ndipo wakavamia eneo hilo.

    Makachero kadha kutoka jijini Nairobi walifanya upelelezi wao ambapo walifuata lori lililobeba bidhaa gushi ambapo lilikamilisha safari yake katika kampuni ya African Spirit mjini Thika. Uchunguzi zaidi unaeleza kuwa kampuni hiyo ya African Spirits Distillers Ltd ndiyo hutengeneza pombe aina ya Blue Moon, na Legends.

    Baada ya kufanya upekuzi zaidi maafisa hao walipata lita 10,000 za kemikali aina ya ethanol, na vibandiko bandia vya KRA.

    Alisema watazidi kushirikiana na idara ya KRA ili kuona ya kwamba watu wanaofanya mambo kwa njia ya mkato wanatiwa nguvuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako