• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi    Jina lingine analoitwa Xi Jinping

  (GMT+08:00) 2019-02-08 08:09:09

  Mbele ya watoto, Xi Jinping anajiita ni "Rafiki mkubwa" wa watoto, na anafuatilia sana ukuaji wa vijana na watoto, na kufuatilia suala la elimu ya vijana na watoto. Alipotembelea shule aliyowahi kusoma, aliwaambia walimu kwamba, "Nimefika shuleni hapa, msiniite kiongozi, sote ni wanafunzi wenu sasa". Xi Jinping anawaheshimu walimu na kuwashukuru walimu, na anawatia moyo na kuwataka wafanye juhudi zaidi kuendeleza mambo ya elimu, yote hayo yamekuwa nguvu ya kusukuma mbele maendeleo ya mambo ya elimu. Katika kipindi hiki cha "Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi", leo tunawaletea makala ya nne ya "Jina lingine analoitwa Xi Jinping".

  "Siku ya Watoto ya kimataifa ya Juni Mosi inakaribia, mimi nikiwa rafiki mkubwa wa watoto, ninawatakia vijana na watoto wote wa makabila yote wa China heri ya sikukuu."

  Huo ulikuwa mwaka 2013, Rais Xi Jinping aliwatakia vijana na watoto wa nchi nzima heri ya Siku ya Watoto ya Juni Mosi. Kipindi cha utoto ni kipindi chenye thamani kubwa zaidi kwa maisha ya kila mtu, alipokutana na watoto, Rais Xi anawaelezea mambo mengi aliyopitia alipokuwa mtoto, na kuwataka watoto waweze kupata mwamko kutokana na maelezo yake. Wakati wa mkesha wa Siku ya watoto ya Juni Mosi mwaka 2014, Rais Xi alitembelea Shule ya msingi ya makabila madogomadogo ya Eneo la Haidian mjini Beijing, akiwasimuliiua watoto mambo mawili kuhusu maisha ya utotoni mwake.

  "Xi: Nakumbuka kuwa wakati najiunga na kikosi cha chipukizi watoto, moyo ulidunda sana, na nilikuwa na furaha sana. Sijui nyinyi mlikuwa wa namna gani?

  Mtoto: Ni sawa na wewe.

  Xi: Mnaelewa au la? Kwa sababu hii ni heshima tunayopata. Kutokana na furaha mliyonayo, nimeona matumaini, yaani matumaini ya nchi yetu na taifa letu. Kama tulivyoapa wakati wa kujiunga na kikosi cha watoto, ni lazima wote wako tayari wakati wowote, ili wafuate nyayo za watangulizi."

  Tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama ufanyike, Xi Jinping amekuwa anasherehekea kila mara Siku ya watoto ya kimataifa na vijana na watoto, na kutoa maagizo kwa watoto. Akisema:

  "Vijana kuwa na nguvu ni jambo muhimu sana, ni lazima mjikakamue na kuwa na nia imara tangu utotoni. Kwa sababu maendeleo ya nchi yanategemea juhudi za watu kizazi hadi kizazi na, watu wenye nguvu kubwa zaidi kizazi hadi kizazi, ili nchi yetu iweze kuwa na nguvu kubwa z siku hadi siku. Fanyeni juhudi zaidi, watoto wetu!"

  Wakati wa mkesha wa Siku ya walimu mwaka 2016, Xi Jinping alirudi katika Shule ya Ba Yi ya Beijing, ambayo ni shule ya msingi na ya sekondari aliyosoma, ambapo alikutana kwa furaha na mwalimu wake Chen Qiuying, na walimu wengine kadhaa akikumbuka pamoja na walimu wao mambo yaliyopita utotoni mwake. Akisema:

  "Leo natembelea tena shule niliyosoma, nimeona kila kitu cha zamani hapa kinagusa sana hisia zangu, sasa mabadiliko makubwa yametokea shuleni, lakini bado ninakumbuka sana kipindi niliposoma hapa, bado ninakumbuka mafunzo ya walimu, mienendo ya shule, na ushawishi wa misingi ya uendeshaji wa shule kwa sisi wanafunzi."

  Machoni mwa Rais Xi Jinping, "Elimu ni msingi wa mpango wetu wa miaka mia moja. Na walimu ni msingi wa kuendeleza elimu, walimu wanabeba jukumu kubwa la kumwezesha kila mtoto akue vizuri, na kuendesha mambo ya elimu ili wananchi waridhike nayo." Akisema:

  "Mtu akikutana na walimu wazuri, hii ni bahati kwake, shule ikiwa na walimu wazuri, ni fahari kwa shule, na kama walimu wazuri watajitokeza bila kusita, hayo ni matumaini ya taifa. Ni lazima walimu wote wawe viongozi wa wanafunzi katika njia ya kujijengea mienendo na kusoma, ili wawe hodari na kutoa mchango kwa ajili ya taifa katika siku za baadaye."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako