• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaahidi kuboresha mazingira ya biashara

    (GMT+08:00) 2019-02-08 09:32:51

    Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameahidi kuwa serikali itaendelea na nia yake ya kuboresha mazingira ya biashara na kurahisisha uwezekezaji wa ndani na nje ya nchi.

    Akizungumza bungeni mjini Dodoma waziri Majaliwa amesema hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali zinalenga kuwavutia wawekezaji kwenye fursa zilizopo za uwekezaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

    Amesema Tanzania ina ardhi ya kutosha kurahisisha aina yoyote ya uwekezaji ambapo mabaraza ya miji yameelekezwa kutenga maeneo maalumu ya ardhi kwaajili ya shughuli za uwekezaji.

    Amefafanua kuwa rais John Magufuli amekuwa akifanya mikutano na mabaraza ya miji kama sehemu ya juhudi za kuhakikisha yanakuwepo mazingira mazuri ya biashara. Mbali na hapo amesema hatua zimechukuliwa za kuboresha miundo mbinu, ikiwemo barabara na bandari, na ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako