• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa AU kuangalia hali ya wakimbizi wa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-02-08 09:33:28

    Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika jana walikutana katika makao makuu ya Umoja huo huko Addis Ababa, Ethiopia kujadili hali ya wakimbizi wa Afrika, wakimbizi waliorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani.

    Katika mkutano huo wa siku mbili ambao unamalizika leo, mawaziri hao wanatarajiwa kuangalia kwa kina ufumbuzi muhimu wa kudumu kwa wakimbizi wa Afrika na msukosuko wa wakimbizi, na kuandaa mapendekezo kwaajili ya mkutano mkuu wa wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Afrika unaotarajiwa kufanyika Februari 10 na 11. Kwenye hotuba yake ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamt amesemea kikao hicho cha baraza la utendaji, kitajadili ufumbuzi wa msukosuko wa wakimbizi.

    Habari zaidi zinasema China na Umoja wa Afrika wamesisitiza kuimarisha ushirikiano kwenye masuala ya amani na usalama kupitia utekelezaji wa mafanikio wa Mpango wa Amani na Usalama wa China na Afrika. Kwenye mazungumzo yake na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Afrika, msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Chen Xiaodong amesema China inatarajia mazungumzo hayo yatajenga ushirikiano katika kufikiria na kuchukua hatua kati ya pande mbili, na kutoa ushauri wa namna ya kutekeleza mpango wa amani na usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako