• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe yupo tayari kwa mazungumzo na Upinzani

    (GMT+08:00) 2019-02-08 17:15:47

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema yupo tayari kukutana na vyama vya siasa vya upinzani nchini humo kwa mazungumzo ya kitaifa ili kuleta maendeleo.

    Mnangagwa juzi Jumatano alikutana na wagombea 20 wa urais wa uchaguzi wa mwaka jana na kujadili mfumo wa uchaguzi ujao wenye lengo la kutatua matatizo yanayolikabili taifa hilo.

    Amesema mkutano huo ulikuwa kutimiza ahadi aliyoitoa wakati alipoapishwa kuingia madarakani mwezi Agosti mwaka jana ya kuwashirikisha wapinzani wa kisiasa kuhimiza kusonga mbele maendeleo ya nchi hiyo.

    Naye mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Zimbabwe Bishow Parajuli amewashukuru viongozi wa upinzani kwa kukubali mazungumzo hayo kama njia ya kukabiliana na matatizo makubwa ya kiuchumi, na kuongeza kuwa majadiliano hayo yatatoa matumaini ya amani na umoja, na kuwa ni muhimu mchakato huo haukuingiliwa na mataifa ya nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako