• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jean Juncker asisitiza Umoja wa Ulaya hautafanya mazungumzo mapya kuhusu makubaliano ya BREXIT na Uingereza

  (GMT+08:00) 2019-02-08 17:22:35

  Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean Juncker jana huko Brussels amesema, Umoja wa Ulaya hautafanya mazungumzo mapya na Uingereza kuhusu makubaliano ya BREXIT, lakini unapenda kurekebisha mambo kuhusu uhusiano wa siku za usoni kati ya Umoja wa Ulaya na Uingereza yaliyomo kwenye taarifa ya kisiasa ya mfumo wa uhusiano kati yao.

  Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May jana aliwasili Brussels, kukutana na Bw. Jean Juncker, mwenyekiti wa baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk, spika wa bunge la Ulaya Antonio Tajani na viongozi wengine kuhusu kuanzisha tena mazungumzo ya makubaliano ya BREXIT.

  Kwenye taarifa ya pamoja, Bw. Jean Juncker amesisitiza kuwa, usuluhishi wowote unapaswa kukubaliwa na bunge la Ulaya na nchi wanachama 27 wengine wa Umoja wa Ulaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako