• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya ulinzi ya Russia yahimiza Marekani kurudi kwenye makubaliano ya makombora ya masafa ya kati

    (GMT+08:00) 2019-02-08 18:19:21

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Russia Igor Konashenkov amesema, wizara hiyo imewasiliana na ofisa wa kijeshi wa ubalozi wa Marekani nchini humo na kupendekeza Marekani kuchukua hatua kurudi kwenye makubaliano ya makombora ya masafa ya kati.

    Bw. Konashenkove amesema, Russia inapendekeza Marekani kufuata makubaliano hayo na kuteketeza vituo vya MK-41 vya kurusha makombora ya aina ya Tmahawk. Pia amesema, Russia inakanusha tuhuma yoyote ya Marekani dhidi yake ya kukiuka makubaliano hayo.

    Habari zinasema, wizara ya ulinzi ya Russia iliwahi kupenda kufanya mazungumzo na Marekani kuhusu makubaliano hayo. Lakini Marekani haijatoa uthibitisho wowote kuhusu tuhumu yao wala kuondoa vitendo vyao vya kukiuka makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako