• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Meli ya kwanza kutia nanga Lamu mwezi Novemba

    (GMT+08:00) 2019-02-08 18:38:29
    Meli ya kwanza kabisa inatarajiwa kutia nanga katika bandari ya Lamu mwezi Novemba mwaka huu.

    Mwenyekiti wa mradi wa LAPSSET,Ttitus Ibui ambaye alikuwa ameandamana na maafisa wengine katia ziara ya bandari ya Lamu nchini Kenya alisema mradi huo wa ujenzi wa bandari ya Lamu utakamilika kwa wakati.

    Alisema ujenzi wa eneo la kwanza la kuegesha meli katika bandari ya Lamu utakamilika mwisho wa mwezi Juni.

    Serikali inatarajiwa kujenga maeneo matatu ya kwanza kuegesha meli kati ya 32 yatakayojengwa kwa gharama ya Sh48 bilioni.

    Maeneo mengine mawili ya kuegesha meli yanatarajiwa kukamilika kufikia mwisho wa mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako