• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma yalima ekari 800 za korosho

  (GMT+08:00) 2019-02-08 18:44:32

  Wakulima katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wamelima ekari 800 za korosho.

  Haya ni kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabiri Shekimweri.

  Akizungumza na wanahabari jana,Shekimweri alisema wilaya hiyo iliweka mikakati ya kilimo cha zao hilo la biashara ili kuwainua wananchi kiuchumi.

  Alisema wilaya hiyo ilifanya utafiti kwa kuwashirikisha wataalamu wa kilimo cha zao la korosho na kubainisha maeneo yanayostahiki kwa kilimo hicho.

  Aidha alisema kuwa baada ya utafiti huo,ardhi ya vijiji 22 ilionekana kufaa kwa kilimo cha zao hilo.

  Aliongeza kuwa mikakati ya wilaya iliyowekwa ni kuwa kila mwananchi wa vijiji hivyo anatakiwa kulima ekari mbili za korosho.

  Alisema mkakati mwingine ni kuhakikisha kila taasisi na serikali ya kijiji husika wanalima zao hilo ekari zisizopungua 20 kila moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako