• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump na Kim kukutana tena mwisho wa mwezi huu huko Hanoi Vietnam

    (GMT+08:00) 2019-02-09 16:09:50

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema atakutana kwa mara ya pili na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, Februari 27 na 28 huko Hanoi, Vietnam.

    Kwenye ujumbe wake kupitia twita rais Trump amesema mwakilishi wake Stephen Biegun ameondoka Korea Kaskazini baada ya mazungumzo ya kiujenzi na kukubaliana muda na tarehe ya kukutana, na kusisitiza kuwa anatarajia sana kumuona Mwenyekiti Kim na nia yake ya kuboresha amani.

    Mapema siku hiyo, wizara ya mambo ya nje ilitoa taarifa ikisema wakati yupo Korea Kaskazini Bw. Biegun alikutana na mwakilishi maalumu wa Korea Kaskazini anayeshughulikia mambo ya Marekani Bw. Kim Hyok Chol Februari 6 hadi 8, huko Pyongyang. Na pande hizo mbili zilijadili nia ya rais Trump na Mwenyekiti Kim ya kuondoa kabisa silaha za nyuklia, kugeuza uhusiano wa Marekani na Korea Kaskazini, na kujenga amani kwenye peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako