• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa UNECA atoa wito wa kufanyika juhudi za pamoja ili kuwasaidia wakimbizi wa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-02-09 16:10:22

    Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa UNECA, Vera Songwe, jana alitoa wito wa kufanyika juhudi za kuwasaidia wakimbizi na wakimbizi wa ndani katika Afrika nzima.

    Akiongea kwenye kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Afrika, kinachofanyika katika makao makuu ya umoja huo Addis Ababa, Ethiopia amesema kama wakiangalia kwa makini idadi hiyo, wakimbizi milioni 23 wanawakilisha mara mbili ya idadi ya watu wa Tunisia, na ni karibu ya idadi ya watu wa Ivory Coast, ambao wataweza kuondoa mzigo mkubwa wa Afrika wa hivi sasa.

    Bi. Songwe amewataka viongozi hususan wa Afrika kukabiliana kwa pamoja na masuala yanayowathiri wakimbizi vijana wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako