• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watalii kutoka China watilia nguvu ya uhai duniani

  (GMT+08:00) 2019-02-09 16:37:42

  Mashirika husika ya utalii nchini China hivi karibuni yalikadiria kuwa, kwenye kipindi cha sikukuu ya Spring ya mwaka 2019 nchini China, idadi ya wachina watakaotalii nchi nyingine itafikia milioni 7, na kuongezeka kwa asilimia 15 kuliko mwaka 2018. Thailand, Japan na Indonesia na nchi jirani zimekaribishwa zaidi na wachina. Mkurugenzi wa Baraza la utalii duniani (WTTC) anayeshughulikia sera na matangazo Bw. Olivia Ruggles Brise alisema, kuongezeka kwa wachina wanaoweza kubeba gharama za utalii kumehimiza masoko ya nchi jirani ya utalii ya China zikiwemo Bangkok na Jakarta. Ofisa mtendaji wa kampuni moja ya kimataifa ya hoteli Bw. James Riley alisema, amezingatia mabadiliko ya tabia za utalii wa wachina, zamani watalii wa China walikuwa wananunua bidhaa tu, lakini hivi sasa wanapenda kuona utamaduni zaidi.

  Hivi sasa sekta ya utalii imekuwa nguvu kuu ya kuhimiza ongezeko la uchumi. Mwaka 2018 idadi ya watalii ilifikia bilioni 1.4, ambapo imefikia kiwango hicho mapema kwa miaka miwili kuliko makadirio ya shirika la utalii duniani. Hasa watalii kutoka China wanaongezeka kwa utulivu. Mwaka 2014 idadi ya wachina waliotalii nchi nyingine ilizidi milioni 100 kwa mara ya kwanza, na mwaka jana idadi hiyo imefikia milioni 140, wachina walitalii nchi na sehemu 157 duniani. Kuanzia mwaka 2013, China imekuwa nchi kubwa zaidi yenye watalii wanaotembelea nchi nyingine.

  Watalii wa China walitoa mchango mkubwa kwa nchi wanazotalii. Mwaka jana idadi ya wachina waliotalii nchini Indonesia ilifikia milioni 2. Waziri wa utalii wa Indonesia Bw. Arief Yahya alisema kila mtalii wa China anatoa dola za kimarekani 1,100 kwa wastani, na kuwa chanzo kikuu cha nchi hiyo katika kujiingizia fedha za kigeni. Takwimu za Uingereza zinaonesha kuwa, mwaka 2017 watalii wa China walitoa dola za kimarekani bilioni 900, na kuongezeka kwa asilimia 35 kuliko mwaka 2016, hivyo Uingereza inachukulia China kuwa nchi yenye thamani kubwa zaidi ya watalii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako