• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF yatoa wito wa kuwasaidia watoto milioni 13.5 waliohama makwao katika Afrika

    (GMT+08:00) 2019-02-10 16:19:08

    Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetoa wito kwa mataifa ya Afrika kuchukua hatua madhubuti pamoja na kuwa na ushirikiano wa kikanda na kimataifa ili kuendeleza haki za watoto wa Afrika waliohama kwenye makazi yao na kuwasaidia kufikia uwezo wao.

    Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Henrietta Fore na kuwataka viongozi wa Umoja wa Afrika kushirikiana katika kukabiliana na mifumo hasi au uhamiaji usio wa kawaida na kuitikia wito wa mahitaji ya watoto katika Afrika. Amesema Kila siku, watoto na familia wanakabiliwa na vitendo vya kimabavu, umasikini au mabadiliko ya hali ya hewa na kufanya maamuzi magumu ya kuhama makwao wakitafuta usalama na maisha mazuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako