• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu wa rais wa Venezuela amtaka Bw. Guaido asimamishe vitendo visivyo vya kawaida

    (GMT+08:00) 2019-02-10 16:39:25

    Makamu wa rais wa Venezuela Bibi Delcy Rodriguez jana alitoa taarifa akimtaka kiongozi wa chama cha upinzani ambaye pia ni mwenyekiti wa bunge la Venezuela Bw. Juan Guaido asimamishe vitendo visivyo vya kawaida.

    Bw. Guaido juzi alisema kuwa huenda ataikabidhi Marekani au nchi nyingine haki ya kuingilia kati kijeshi mambo ya Venezuela kama ikihitajika, ili kumlazimisha rais Maduro kujiuzulu na kutatua mgogoro wa kibinadamu nchini Venezuela.

    Bibi Rodriguez alisema kuwa, watu wa Venezuela wameonesha matarajio yao ya kutaka amani na utulivu. Pia alisisitiza kuwa misaada ya binadamu ya Marekani ni udhuru wa kuishambulia Venezuela.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako